HISTORIA YA LVBC

Mmishenari Jim Petersen na mkewe wakitoa salaamu siku ya ufunguzi wa chuo

Mnamo mwaka 1994 Mmisionari Jim Petersen aliye kuwepo Mwanza mwaka wa 1994 alinunua eneo hili kwa ajili ya ujenzi wa KITUO CHA MIKUTANO, kwa matumizi ya mikutano na semina mbalimbali. April 2000 Mmishenari Jerry Spain alibadilisha maono ya kuwa kituo cha Mikutano na badala yake kuwa Chuo cha kuwaandaa wachungaji kwa kanda ya ziwa Victoria. Chuo kilianza kupokea rasmi wanachuo mwaka 2001, Chini ya Uongozi wa Mkuu wa Chuo Mchungaji Ron Swai, Rebeka Kakila na Mama Joyce Jarvis walikuwa wakufunzi wa kwanza.

Mwezi Januari 2001 chuo kilianza rasmi na wanafunzi wapatao 33. Miundo mbinu mbalimbali ambayo ilikuwa haijakamilika, iliendelea kuboreshwa kama vile umeme na maji. Mwezi March 2001 ujenzi wa
madarasa ulianza nakukamilika mwezi Mei 2001.

Tarehe 8 Juni, 2001 ulifanyika ufunguzi rasmi wa chuo cha Biblia cha LVBC na aliyekuwa Askofu Mkuu Rev. Ranwell Mwenisongole. Wageni wengine walioambatana na mgeni rasmi walikuwa Rev. Rogathe Swai, aliyekuwa Makamu Askofu Mkuu, Rev.Yusufu Mbelwa, aliyekuwa Katibu Mkuu, Rev. Jothamu Mwakimage aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Elimu. Wageni waalikwa walikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mheshimiwa Stephene Mashishanga, Mmishenari Jim Petersen na mke wake kutoka Zambia aliyeanzisha mradi na Tim na Joyce Jarvis waliokamilisha mradi. Wageni wengine walikuwa ni askofu wa jimbo Mchungaji. Jason Lugwisha na wachungaji wengine wengi walihudhuria siku hiyo.

Mgeni Rasmi Askofu Mkuu Rev. Ranwell Mwenisongole, mbele katikati akiongozana na Makamu Askofu Mkuu Rev. Rogathe Swai kushoto na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mheshimiwa Stephene Mashishanga
wakiongoza maandamano kuingia chuoni.

Askofu mkuu wa Tanzania Assemblies of God akiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Elimu katika sherehe za Uzinduzi wa Bweni jipya la kisasa la Wanawake.

Maendeleo ya Chuo

Chuo kiliedelea vizuri na miundo mbinu kama vile umeme na maji iliendelea kupatikana hatua kwa hatua. Mwaka 2003 ujenzi wa bweni moja la wanaume lenye uwezo wa kulaza watu 64 ulianza hadi mwaka 2004 ulikamilika. 

Baadaye Mungu alianza kufungua milango zaidi ambapo nyumba za walimu zilianza kujengwa mwaka 2005 na kuwa na nyumba za kutosha walimu saba. Pia idadi ya wanafunzi iliendelea kuongezeka kwa wanafunzi waliokuwa wanajiunga na chuo. Chuo kiliwahi kuvunja rekodi ya kupokea wanachuo wapya wapatao 77 kwa mara moja mwaka 2010, na kufanya idadi ya wanachuo kufikia 115 mwaka huo.

Pia ujenzi wa bweni la kisasa la wanawake lenye uwezo wa kuchukua watu 32 ulianza na kukamilika.

Mwaka 2003 ilifanyika sherehe kubwa ya mahafali ya kwanza. Wahitimu wa kwanza wapatao 30;
wanaume 26 na wanawake 4 walitunukiwa stashada zao. Ilikuwa ni siku kuu ya kihistoria ya kukumbukwa
kwa kutimia maono ya mtumishi wa Mungu Jerry Spain aliyetamka kuwa mahali hapa pangekuwa chuo cha
kufundisha watumishi wa Mungu.

Historia Wakuu wa Chuo LVBC

0987654321